Nukuu za alichokisema Wema Malisa baada ya kufukuwa na Polisi Juni 18, 2013 katika Uwanja wa Soweto, Arusha ambapo watu kadhaa walikukusanyika ili kuwaaga watu wanne waliokufa kwenye mlipuko wa bomu katika mkutano wa CHADEMA, Jumamosi ya Juni 15, 2013 katika uwanja uo huo.
Picture: Wema Malisa
Wema Malisa
Nilikuwa namfuata baba yangu ambaye ni kada wa CHADEMA. Kutokana na ulemavu wake nilihofu angepata matatizo kama vurugu zingezuka.

Nilikuta uwanja ukiwa umefurika wananchi wakiwasikiliza viongozi wa Chadema. Viongozi hao ni Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye alihutubia na kumwachia Tundu Lissu naye akamwachia Said Arfi. Alipomaliza kuwataka wanachama hao waelekee Hospitali ya Mount Meru, ndipo mabomu yakaanza kulipuliwa.

Nilimwambia baba tuondoke lakini tulikuwa tumeshachelewa, polisi walikuwa wametuzingira. Bomu la pili liliangukia mbele yetu. Askari mmoja akasema ‘laleni chini’, tukalala tukidhani 
tutakuwa salama. Lakini walikuja askari na kutupiga marungu mwili mzima mimi na baba.

Ghafla akatokea askari mwingine akawakataza wasitupige, tukadhani tumeokoka. Mara wakatokea askari wengine, hapo ndipo kilikuwa kipigo kitakatifu. Nilijaribu kuwazuia wasimpige baba kwa kuwa ni mlemavu, wakanikebehi kuwa huyo ni hawara yangu. Walinipiga mpaka mkono na mguu ya kushoto ikavunjika.

Tulikuwa kwenye kibaraza cha nyumba wakati askari wanatupiga. Askari mmoja alirarua gauni langu chini na juu, hadi nikabaki uchi mbele ya baba. Mwingine akakoki bunduki na kuielekeza katikati ya mapaja yangu ili alipue sehemu za siri, wenzake wakamkataza. Mwingine alisema kuwa atanibaka. Baba alinikumbatia akasema watuue wote, mimi niliomba wasituue maana nimeacha mtoto mchanga nyumbani.

Walisema ‘unajifanya wewe CHADEMA, sasa ndiyo utajua kuwa CCM inatawala. Chezea CCM wewe.’ Mimi niliwaambia sina chama chochote nimekuja kumwokoa baba yangu. Wakati huo wote walishanivua hereni, simu wakachukua na fedha zilizokuwa ndani ya pochi na kuitupa chini ikiwa tupu.

Alitusikitikia na kusema, ‘kwa nini mnang’ang’ania kuwa Chadema? Angalieni sasa mlivyoumia na viongozi wenu wamewakimbia.’ Akaokota kanga iliyoachwa uwanjani na kuja kunifunika... Kisha likaja gari la polisi tukabebwa na kuingizwa humo. Mwendo tuliondoka pale ulikuwa wa kasi huku wakiendelea kulipua mabomu na kutukanyaga bila kujali. Tulishtukia tuko Hospitali ya Mount Meru, tukabwagwa hapo na gari hilo likaondoka.
KAULI YA Mzee Malisa
Kilichonisikitisha ni kitendo cha kumpiga na kumdhalilisha mwanangu mbele yangu. Askari wengine walikuwa wakijaribu kuvunja hili gongo ninalotembelea kwa sababu ya ulemavu

Nimesikitishwa na kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyoitoa hivi karibuni Bungeni Dodoma ya kuwataka askari waendelee kupiga wananchi. Kwa hali hii sisi wanyonge natuna pa kukimbilia.”
Nukuu kutoka kwenye habari katika gazeti: Mwananchi


Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/06/ya-arusha-askari-mmoja-alirarua-gauni-langu-nikabaki-uchi-mbele-ya-baba.html#ixzz2XE5epVQG

Comments

Popular posts from this blog

happy clients arrived at kilimanjaro airport - take a look at the video.

Kilimanjaro climb 9days ( 7days of climb ) 2pax in a joining group:

we can Possibly take you to Nairobi -Kenya please see the Itinerary and request for cost /rate